Tovuti zinazouza
Kwa Kiswahili na Kiingereza, zinafunguka haraka kwenye simu, na zinaleta wateja moja kwa moja kupitia WhatsApp na Google.
Ninajenga tovuti na mifumo salama inayochukua nafasi ya madaftari, Excel na kamisheni kubwa — kwa hoteli, migahawa, shule na SACCOS.
Oda za karatasi zinapotea, na wateja wanasubiri.
Kila booking ya mtandaoni inapita kwa mtu wa kati na kamisheni yake.
Stoo na mauzo vinahesabiwa kwa mkono mwisho wa siku.
Tovuti ya zamani haifunguki vizuri kwenye simu, wala haina usalama.
Imejengwa kwa jinsi unavyofanya kazi, inajaribiwa na watakaoitumia, na ni mali yako.
Kwa Kiswahili na Kiingereza, zinafunguka haraka kwenye simu, na zinaleta wateja moja kwa moja kupitia WhatsApp na Google.
Wageni wanabook na kulipa kwa M-Pesa au kadi moja kwa moja kwako, bila kamisheni ya mtu wa kati.
POS, stoo, ada za shule, michango ya SACCOS — namba zako kwa wakati halisi, badala ya madaftari matano.
Ninaangalia jinsi biashara yako inavyofanya kazi leo, na gharama halisi ya njia ya sasa. Kisha tunaamua pamoja: tuendelee au tusiendelee.
Michoro unayoikubali kwanza, kisha ujenzi. Unaona maendeleo kila wiki, na wafanyakazi wako wanaijaribu kabla ya kuzinduliwa.
Mafunzo kwa timu yako, domain na code kwa jina lako, na dhamana ya siku 30.
Baada ya siku 60 tunapima matokeo pamoja: muda uliookolewa, oda, booking za moja kwa moja.
Jaribu demo ya oda kwa QR — kama mteja wako angeiona kwenye simu yake.
Tovuti inayoeleza programu, maeneo ya kazi na timu, yenye njia za kuchangia, kujitolea na kushirikiana, pamoja na fomu ya mawasiliano na WhatsApp.
Mteja anascan QR mezani, anaagiza kwenye simu yake, na jikoni wanaona oda papo hapo kwenye dashboard.
Mfumo wa stoo, mauzo na ankara wenye tahadhari za dawa zinazokaribia kuisha muda na ripoti za kila siku.
Mfumo wa kusajili sampuli, kufuatilia vifaa na kutoa ripoti safi kwa uongozi.
Bei kamili hutolewa baada ya mazungumzo ya bure, kulingana na mahitaji yako.
Kwa biashara inayotaka kuonekana mtandaoni.
TSh 350k+
Kwa hoteli, migahawa na biashara zinazopokea wateja mtandaoni.
TSh 800k+
Mfumo unaojengwa kwa jinsi biashara yako inavyofanya kazi.
TSh 2.5M+
Hosting na domain
TSh 30,000 – 60,000 / mwezi
Tovuti inakaa hewani, na email ya biashara kwenye domain yako.
Matengenezo
TSh 50,000 – 150,000 / mwezi
Masasisho, backup, ufuatiliaji wa usalama na saa 2 za mabadiliko kila mwezi.
Msaada wa mfumo
TSh 150,000 – 400,000 / mwezi
Kwa mifumo maalum: msaada wa watumiaji, marekebisho na maboresho madogo.
Bure · dakika 2 kujaza · hakuna masharti.
Nakagua tovuti ambazo mwombaji ni mmiliki au ana ruhusa ya mmiliki tu.
Wewe. Domain inasajiliwa kwa jina la biashara yako, na unapata access zote mara malipo yanapokamilika.
50% kabla ya kuanza na 50% kabla ya tovuti kwenda hewani. Kwa mifumo mikubwa tunaweza kugawanya malipo kwa awamu tatu. Unaweza kulipa kwa simu au benki.
Kifurushi cha Msingi ni wiki 1–2, Biashara wiki 3–4, na mifumo maalum kuanzia wiki 6. Muda unategemea pia jinsi picha na maandishi yanavyopatikana haraka.
Ndiyo. Tunaanza na ukaguzi wa bure wa usalama na kasi, kisha nakupa mapendekezo na bei ya kuiboresha au kuijenga upya.
Dhamana ya siku 30 inashughulikia hitilafu bila malipo. Baada ya hapo, mpango wa matengenezo unakupa backup, masasisho ya usalama na msaada.
Inategemea. Tovuti za kawaida zinaweza kutumia WordPress ili uweze kubadilisha maudhui mwenyewe; mifumo maalum inajengwa kwa code ili iwe salama na ifanye kazi kama biashara yako inavyohitaji.
Ninajibu ndani ya siku 1 ya kazi. Taarifa zako hazitumwi kwa mtu mwingine.
Unahitaji nini?
Chagua moja, na WhatsApp itafunguka na ujumbe tayari.